Uislamu ni dini ya nidhamu

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewasisitiza Waislamu nchini kuachana na tabia ya kugombania misikiti, kwani haisaidii kuendeleza dini hiyo. Amesema misikiti ni nyumba za Mwenyezi Mungu, hivyo hakuna sababu kwa Waislamu kulumbana kwa sababu za kugombea uongozi au kutokana na tofauti ya kimadhehebu.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria  ufunguza wa MASJID AQSAA katika kijiji cha Kiboja Mkwajuni, Wilaya ya Kati Unguja. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria ufunguza wa MASJID AQSAA katika kijiji cha Kiboja Mkwajuni, Wilaya ya Kati Unguja.

View original post 473 more words

Advertisements

TALAKA KATIKA UISLAMU

بسم الله الرحّمن الرّحيم

الطلاق في الإسلام .

TALAKA KATIKA UISLAMU.

Baada ya kumshukuru ALLAH (SW) kama anavyostahiki kushukuriwa, sala na salamu zimfikie Mjumbe wake Sayyidina Muhammad (saw) pamoja na Masahaba wake na kila anaefuata njia yake kwa wema mpaka siku ya malipo.

Amma baad :

Enyi Waja wa ALLAH :

Mshukururuni na mdhukuruni ALLAH (SW) kwa neema zake nyingi juu yenu. Na katika neema hizo ni neema ya ndoa ambayo ni mafungamano madhubuti na ya halali baina ya mwanamme na mwanamke, yenye kuhifadhi viungo kutokana na uchafu wa zinaa na yenye kujenga nasabu njema.

ALLAH (SW) amewataka watu wote washikamane na mwendo huu ili wapate kumuogopa na kuzishukuru neema zake pale aliposema :

{ يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُواْ رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالاً

كَثِيراً وَنِسَاءً } سورة النّساء 1

“ Enyi Watu ! Mcheni Mola wenu ambae amekuumbeni kutoka katika nafsi moja.

Na akaumba mkewe kutoka katika nafsi hiyo. Na akaeneza wanaume wengi

na wanawake kutoka katika wawili hao. ”.

ALLAH (SW) anaendelea kutueleza matunda ya mafungamano haya mema kwa kusema :

{ وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجاً لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِيْ

ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ } سورة الروم 21

“ Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, nae amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila ya shaka katika hayo, zimo ishara kwa watu wanaofikiri ”.

Ndugu Waislamu.

Hapana shaka kuwa maisha ya ndoa yana mitihani na matatizo yake, lakini kutokana na umuhimu wake Uislamu umeweka hikma na njia nyingi za kuyalinda ili yapate kudumu na kuendelea. Ndio tukaona kuwa katika Kitabu cha ALLAH kuna aya nyingi zinazotufahamisha nini cha kufanya pale yanapotokea matatizo baina ya mume na mke.

– Kwanza anatakiwa mume amnasihi mke wake, na kama nasaha hazikutosha basi ajitenge nae katika malazi, na kama itabidi anaruhusiwa hata kumpiga, lakini kipigo hicho kiwe kidogo na kisicholeta madhara.

Anasema ALLAH (SW) :

{ وَاللاَّتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلاَ

تَبْغُواْ عَلَيْهِنَّ سَبِيلاً إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيّاً كَبِيراً } النساء 34

“ Na wanawake ambao mnaona uasi wao kwenu, wanasihini na waacheni pekee yao katika vitanda na wapigeni. Na wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bila ya sababu. Hakika ALLAH ndie alie juu na mkuu ”.

– Iwapo mume na mke watashindwa kutatua matatizo yalioko baina yao, basi njia ya pili itakua ni kutafuta sulhu kwa kutumia wapatanishi kutoka katika familia za mume na mke.

Anasema ALLAH (SW) :

{وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُواْ حَكَماً مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَماً مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلاَحاً يُوَفِّقِ اللّهُ

بَيْنَهُمَا إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيماً خَبِيراً } النساء 35

“ Na kama mkijua kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi mmoja katika jamaa za mwanamme na mmoja katika jamaa za mwanamke. Kama wakitaka mapatano ALLAH atawawezesha. Hakika ALLAH ni mjuzi na mwenye khabari zote ”.

Enyi Waja wa ALLAH.

Pale itapokuwa njia zote za sulhu hazikuweza kutatua matatizo yalioko baina ya mume na mke basi hapo tena ndio itabidi itumike talaka, ambayo ni katika halali inayochukiwa sana na ALLAH (SW).

Amesema Mtume (saw) :

(( أَبْغَضُ الْحَلاَلِ إِلَى اللهِ تَعَالَى الطَّلاَقُ ))

“ Halali inayochusha zaidi mbele ya ALLAH Mtukufu ni talaka ”.

Lakini talaka nayo ina kanuni na sharia zake, na wala sio kitu chepesi na cha mchezo kama waonavyo wengi katika watu.

Kwanza inampasa mume auzingatie wakati wa kutoa talaka, kwani talaka haitolewi wakati wowote tu. Mwanamke hapewi talaka anapokuwa katika hedhi wala anapokuwa katika kipindi cha usafi ambacho ameshawahi kukutana na mumewe.

Anasema ALLAH (SW) :

{ يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ } الطلاق 1

“ Ewe Nabii ! Mtakapowapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao ( yaani baada ya kumaliza hedhi na kabla hamjawingilia ) ”.

Inasimuliwa kuwa Sayyidina Umar ibnu Al-Khattab (ra) alikwenda kwa Mtume (saw) akasema : “ Hakika (mwanangu) Abdullah amemuacha mkewe nae yuko katika hedhi ”.

Akasema Mtume (saw) :

(( مُرْهُ فَلْيُرَاجِعْهَا حَتَّى تَطْهُرَ ثُمَّ تَحِيْضَ ثُمَّ تَطْهُرَ ، فَإِنْ شَاءَ أَمْسَكَ وَإِنْ شَاءَ طَلَّقَ قَبْلَ أَنْ يَمَسَّ

   فَتِلْكَ الْعِدَّةُ الَّتِيْ أَمَرَ اللهُ أَنْ تُطَلَّقَ لَهَا النِّسَاءُ ))

“ Muamrishe amrudie mpaka atahirike kisha apate hedhi kisha atahirike tena, baada ya hapo akitaka atakaa nae na akitaka atamuacha lakini kabla ya kumgusa, kwani huo ndio wakati ambao ALLAH ameamrisha waachwe wanawake ndani yake ”.

Jambo la pili lakuzingatia ni idadi ya talaka zinazotolewa wakati wa kuacha, kwani imekua ni kawaida kwa watu wajinga kutamka idadi kubwa ya talaka wanapoacha ( tatu, kumi, mia ), ingawa talaka inasihi lakini kufanya hivi ni makosa. Hivyo katika sharia, talaka hutolewa moja baada ya moja na sio sawa kuzitoa zote kwa pamoja.

Anasema ALLAH (SW) :

{ الطَّلاَقُ مَرَّتَانِ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ } البقرة 229

“ Talaka ni mara mbili, kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa uzuri ”.

Inasimuliwa kuwa Mtume (saw) alipata khabari ya mtu aliemuacha mkewe talaka tatu kwa pamoja, basi alighadhibika sana kisha akasema :

(( أَيُلْعَبُ بِكِتَابِ اللهِ وَأَنَا بَيْنَ أَظْهُرِكُمْ ))

“Jee kinachezewa kitabu cha ALLAH na bado mimi niko pamoja na nyinyi ? ”

Ndugu Waislamu.

Katika mambo yanayosikitisha siku hizi ni kuwa vijana wengi wamekuwa na tabia ya kuoa na kuacha bila sababu kwa kuchezea mali walizonazo. Hawa hawana shukurani juu ya neema walizopewa na ALLAH (SW), na wanaingia katika kundi la waonjaji ambao wamelaaniwa na Mola wao.

Amesema Mtume (saw) :

(( لَعَنَ اللهُ الذَّوَّاقِيْنَ وَالذَّوَّاقَاتِ ))

“ ALLAH amewalaani waonjaji wanaume na waonjaji wanawake ”.

 

Na kwa upande wa pili wapo wanawake wanaodai talaka bila ya kufanyiwa ubaya wowote na waume zao. Basi hawa na wakumbuke kauli ya Mtume (saw) isemayo :

(( أَيُّمَا امْرَأَةٍ سَأَلَتْ زَوْجَهَا طَلاَقًا مِنْ غَيْرِ بَأْسٍ فَحَرَامٌ عَلَيْهَا رَائِحَةُ الْجَنَّةِ ))

“ Mwanamke yoyote atakaemdai mumewe talaka bila ya kufanyiwa ubaya wowote, basi itakua ni haramu kwake kupata hata harufu ya pepo ”.

Bali wapo wanawake wanaodai talaka kutokana na wivu wa ukewenza tu wakafika hadi kuwaambia waume zao : “ Chagua mmoja mimi au yeye ”. Jee mabibi hawa wamepata wapi mamlaka ya kuharamisha kile alichokihalalisha ALLAH (SW) ? Kwani hawakubali kuwa Mola wetu Mtukufu anasema :

{ فَانكِحُواْ مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَى وَثُلاَثَ وَرُبَاعَ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلاَّ تَعْدِلُواْ فَوَاحِدَةً } النساء 3

“ Basi oweni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. Na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu (baina yao) basi oweni mmoja tu ”.

Na amesema Mtume (saw) :

(( لاَ يَحِلُّ لاِمْرَأَةٍ تَسْأَلُ طَلاَقَ أُخْتِهَا لِتَسْتَفْرِغَ صَحْفَتَهَا فَإِنَّمَا لَهَا مَا قُدِّرَ لَهَا ))

“ Haijuzu kwa mwanamke kudai talaka ya ndugu yake ili apate kumkatia rizki yake katika maisha ya ndoa, kwani hakika yeye atapata kile alichokadiriwa ”.

Enyi Waja wa ALLAH.

Wanawake walioachwa (ambao kisharia wanaweza kurudiwa) wanatakiwa wakae eda katika zile zile nyumba za waume zao, sio ruhusa kwa waume kuwafukuza na wala sio ruhusa kwa wao kuondoka katika nyumba hizo, kwani kwa kule kukaa pamoja huenda ALLAH akajaalia warudiane.

Anasema ALLAH (SW) :

{ وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلاَثَةَ قُرُوءٍ } البقرة 228

“ Na wanawake walioachwa wasubiri mpaka tahara ( au hedhi ) tatu zipite ”.

 

Anasema ALLAH (SW) :

{ لاَ تُخْرِجُوهُنَّ مِن بُيُوتِهِنَّ وَلاَ يَخْرُجْنَ } الطلاق 1

“ Msiwatoe katika nyumba zao na wala wasitoke wenyewe ”.

Na waume zao watakuwa na haki ya kuwarejea katika huo muda wao wa eda.

Anasema ALLAH (SW) :

{ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَلِكَ إِنْ أَرَادُواْ إِصْلاَحاً } البقرة 228

“ Na waume zao wana haki zaidi ya kuwarejea katika muda huo, kama wakitaka kufanya sulhu ”.

Enyi Waja wa ALLAH :

Mcheni ALLAH Mola wenu Mtukufu, mshukuruni kwa neema zake nyingi juu yenu, zichungeni sana ndoa zenu kwa kujiepusha na talaka za mchezo. Wapeni watoto wenu malezi mazuri kwa kuwapa fursa ya kuishi pamoja na wazazi wao wawili.

Na zingatieni vipi inakuwa hali ya maisha ya watoto ambao wazazi wao wameachana.

Kaeni na wake zenu kwa wema kwani Mtume (saw) amesema :

(( اِتَّقُوا اللهَ فِيْ النِّسَاءِ ، فَإِنَّكُمْ أَخَذْتُمُوهُنَّ بِأَمَانَةِ اللهِ وَاسْتَحْلَلْتُمْ فُرُوجَهُنَّ بِكَلِمَةِ اللهِ ))

“ Muogopeni ALLAH katika wanawake, kwani hakika nyinyi mumewaoa kwa amana ya ALLAH na mmejihalalishia tupu zao kwa neno la ALLAH ”.

Na amesema :

(( لَيْسَ مِنَّا مَنْ خَبَّبَ امْرَأَةً عَلَى زَوْجِهَا ))

“ Hayuko katika sisi yule anaeharibu mahusiano yalioko baina ya mwanamke na mumewe ”.

Na pia amesema :

(( تَزَوَّجُوْا وَلاَ تُطَلِّقُوْا ))

“ Oweni na wala msitoe talaka ( bila ya sababu ) ”.

Na amesema :

(( خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لأَهْلِهِ وَأَنَا خَيْرُكُمْ لأَهْلِيْ ))

“ Mbora wenu ni yule mwema wenu kwa watu wake, na mimi ni mwema wenu kwa watu wangu ”

والسلام عليكم ورحمة الله تعالى وبركاته .

Bilaal Bin Rabaah (Radhiya Allaahu ‘Anhu)

Zanzibar Yetu

Bilal-ibn-RabaahMuhammad Faraj Salim As-Sa’ay

‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa kila linapotajwa jina la Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) akisema; “Bwana wetu aliyemkomboa Bwana wetu”. Akimkusudia Bilaal bin Rabaah (Radhiya Allaahu ‘anhu). Wanasema wanavyuoni kuwa; Unapomsikia ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akimwita mtu ‘Bwana wetu’, basi tambua ya kuwa huyo ni mtu adhimu.

Imeandikwa katika Siyar al-A’alaam an-Nubalaa kuwa Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye asili yake ni Mhabeshi (mu-Ethiopia), alikuwa mweusi sana, mwembamba, mrefu na mwenye nywele ndefu.

View original post 2,443 more words

Kumekucha Uchaguzi Mkuu 2015, Lowassa atikisa CCM, upinzani

Zanzibar Yetu

viongozi wa vyama na Serikali nchini Tanzania ambao majina yao yanatajwa na  wananchi kuwa wanaweza kuwania nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu mwakani. viongozi wa vyama na Serikali nchini Tanzania ambao majina yao yanatajwa na wananchi kuwa wanaweza kuwania nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu mwakani.

Dar es Salaam. Kumekucha. Pengine hilo ndilo neno linalofaa kutumika kuelezea matokeo ya utafiti kuhusu kinyang’anyiro cha urais katika Uchaguzi Mkuu 2015 ambayo yanaonyesha kuwa iwapo ungefanyika leo, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa angeibuka mshindi.

View original post 294 more words

Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah

Zanzibar Yetu

hajj_2014

Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa neema Aliyotujaalia ya kutuwekea miezi mitukufu, au siku tukufu au nyakati tukufu ambazo vitendo vyake vyema huwa na thawabu nyingi sana. Na hivi tunakaribia kabisa kuingia katika mwezi mwingine mtukufu wa Dhul-Hijjah. Katika mwezi huu, siku kumi za mwanzo ni siku bora kabisa katika dunia na zina fadhila kubwa kutokana na dalili zifuatazo: 

View original post 2,485 more words

Tangazo: Nafasi za Masomo ya Juu kupitia ufadhili wa Serikali ya Oman

Zanzibar Yetu

Sohar Versity Announcement for Postgraduate Scholarship offered by the Oman Academic Fellowship (OAF) Program for the Academic year 2014/2015

The Ministry of Education and Vocational Training, Zanzibar, in collaboration with the Ministry of Higher Education of Oman and Oman Academic Fellowship (OAF) Joint Committee is pleased to invite potential applicants of qualified Zanzibaris to apply for postgraduate scholarships under the Oman Academic Fellowship (OAF) Program for the academic year 2014/2015.

View original post 355 more words

Hawana Kheri Na Sisi

Zanzibar Yetu

Wakimbizi kutoka Syria wakihifadhi kwenye mahema nchi Lebanon Wakimbizi kutoka Syria wakihifadhi kwenye mahema nchi Lebanon

Na. Naaswir Haamid

Hakika hakuna kiumbe kilichofika duniani kuwatakia wenziwe khayr isipokuwa kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hakutaka mali wala chakula kutoka kwa watu wake. Alielewa lengo lake na hakuingia kwenye ubadhirifu wala ufisadi.

View original post 569 more words