cropped-282299_125368810994226_357495618_n.jpg

ASSALAMU A’LAYKUM WARAHMATULLAHI  WABAKAATUH.

Mpendwa Msomaji wa weblog hii, ninakukaribisha katika jukwaa hili la ZENJIBARZA – Msijitie Kiwewe Zanzibar ina Wenyewe!

Mawasiliano baina yangu, kama msimamizi na mwendeshaji wa weblog hii,  nawe mpendwa msomaji. Pamoja na hayo, weblog hii inatarajiwa iwe jukwaa baina ya Zanzibar na ulimwengu huu mpana ambao sasa umefanywa uwe mwembamba kutokana na njia kama hizi za mawasiliano ya mtandao.

Mimi naitwa Masoud Khamis Hamed Al-Bimani. Ni Mzanzibari niliyezaliwa Mkoani Kisiwani Pemba;Zanzibar. Nina fakhari ya kuzaliwa, kukulia na kuipenda Zanzibar. Kwangu Zanzibar sio tu kwamba ni nchi yangu ya uzawa, bali ni heshima yangu.

ZANZIBAR JIP

Nimepata Elimu yangu ya Msingi katika Skuli ya Ng’ombeni Mkoani Pemba, kuanzia darasa la kwanza Mwaka 1997 hadi darasa la saba Mwaka 2003 .

Kuanzia mwaka 2004 Nilianza masomo yangu ya Sekondari katika Skuli ya Uweleni Mkoani Pemba, hadi Mwaka 2008 Darasa  la Nane (OSC) , Kidato cha Kwanza hadi cha Nne.

Pia katika Mwaka 2009  – 2011 niliendelea na masomo yangu ya Sekondari ya Juu ( Advanced Level) yaani kidato cha tano na sita katika Skuli hiyo hiyo ya Uweleni Mkoani Pemba.

 Kuanzia Mwaka 2011 hadi sasa naendelea na masomo  ya Elimu ya juu katika chuo kinachojuilikana kama COLLEGE OF ISLAMIC SHARIA SCIENCES ambacho kipo maendeo ya AL-KHUWEIR MUSCAT OMAN.

Kutokana na ukweli kwamba mimi ndiye mwanzilishi na muendeshaji wa weblog hii msomaji ategemee kuzipata khabari moto moto zilizohakikiwa na kwa ufanisi wa hali ya juu na waandishi mahiri waliopo ndani na nje ya Zanzibar kwa haraka sana kama zinavyotokea.

Pia katika Menu yetu tumeweka link ya Redio za kimataifa kama vile:

  1. Idhaa ya Kiswahili ya Redio Tehran- Iran.
  2. Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle – Sauti ya Ujerumani.

  3. Idhaa ya Kiswahili ya BBC kutoka London Uingereza.

4.Idhaa ya Kiswahili kutoka Tokyo – Japan.

5.Idhaa ya Kiswahili kutoka Beijing – China.

6.Idhaa ya Kiswahili kutoka Cairo – Misri.

kupitia Weblog hii pia utapata fursa ya kulisoma Jarida la Zanzibar ambalo linatoka kila siku ya Jumapili sambamba na hilo utaweza kusoma Makala zilizoandaliwa na waandishi mbali mbali wa Gazeti la Raia Mwema  pamoja  na Gazeti la Annur Kila Ijumaa.

Vile vile tumeweka link ya Mambo ya Kiislamu in shaa Allah kila unalolihitaji utalipata hapo pia kwa wale wanafunzi wa Lugha ya Kiiengereza na Kiarabu tumewawekea link itakayowasaidia kukuza vipaji na uwezo wao kilugha.

Nina heshima kubwa ya kukaribisha maoni ya kila mchangiaji na naahidi kuheshimu mawazo hayo. Hata hivyo, kwa ajili ya kulinda mila,silka,khulka na desturi adhimu za Kizanzibari, sitachapisha maandishi yoyote yanayokwenda kinyume na utamaduni wetu pamoja na dini yetu ya Kiislam.

Kwa mawasiliano zaidi na mwenye Blog hii tafadhali wasiliana nasi kupitia anuani zifuatazo:

S.L.B : 100,

SIMU: +255 773/715 176 174

Barua pepe: masoudkh7@gmail.com au zenjibarza@gmail.com

Weblogs: https://zenjibarza.wordpress.com , http://uwelenizone.blogspot.com , http://albimany.blogspot.com

UWELENI; MKOANI – PEMBA, ZANIZBAR – TZ.

Kauli mbiu yetu ni

ZANZIBAR NI NJEMA MWENYE HESHIMAZE NA AJE !

                                                                          MSIJITIE KIWEWE ZANZIBAR INA WENYEWE!

Ahsanteni kwa kutuunga mkono!

Advertisements

Toa Maoni yako hapa

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s